Magari ya usafiri wa umma ya chama cha Nicco Movers Matatu Sacco, yameruhusiwa kurejelea shughuli za uchukuzi jijini Nairobi.
Hii ni baada ya Mahakama Kuu kuondoa marufuku iliyokuwa imewekewa chama hicho.
Ilikuwa mapema wiki hii ambapo matatu 159 za chama hicho zinazohudumu kwenye barabara kuu ya Thika ziliwekewa marufuku hiyo.
Matatu hizo zilipigwa marufuku kubeba abiria jijini Nairobi kufuatia kisa cha Juni 5 mwaka huu ambapo abiria mmoja alianguka kutoka mojawapo wa mabasi hayo.
Kesi hiyo itasikilizwa Septemba 21.