Tshisekedi adokeza kuwania Urais kwa muhula wa tatu mwaka 2028

Dismas Otuke
0 Min Read

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi, amesema yuko tayari kuwania muhula  wa tatu afisini katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2028.

Katiba ya sasa haimruhusu Tshisekedi kuwania Urais mwaka 2028, punde atakapokamilisha kipindi chake cha mihula miwili

Hata hivyo,Tshisekedi, amesema endapo raia watapitisha kura ya maoni ya kuongeza muda wa kuhudumu afisini atagombea muhula mwingine.

Katiba ya DRC inamruhusu Rais kuhudumu muhula miwili pekee.

Share This Article