Mahakama Kuu inatarajiwa kutoa uamuzi wa kesi iliyowasilishwa na Seneta wa Busia Okiya Omtatah, ya kupinga kuwepo kwa kituo cha kitaifa cha kujumuisha matokeo ya kura za Urais.
Kwenye kesi hiyo Omtatah anahoji kuwa matokeo ya Urais yanayotangazwa katika eneo bunge ni ya mwisho kulingana na katiba ya mwaka 2010.
Omtatah anataka Mahakama iharamishe na kufutilia mbali kituo cha kitaifa cha kujumuisha matokeo ya kura za Urais.
Licha ya matokeo ya kura za Urais kiwango cha maeneo bunge kuwa ya mwiso,tume huru ya mipaka na uchaguzi (IEBC),imekuwa ikiendesha kituo cha kitaifa cha ujumuishaji kura za Urais katika ukumbi wa Bomas of Kenya kila wa uchaguzi mkuu.