Iran imelalamika vikali baada Marekani kuishambulia, huku tehran ikidokeza kuwa makubaliano ya kusitishwa kwa vita umekiukwa.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema tangu kutangazwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Iran na Marekani tarehe Aprili 8, Marekani imezizuia meli za biashara za Iran baharini, na hivyo kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano.
Kulingana na Wizara hiyo, Marekani itawajibikia vitendo hivyo, ikisisitiza kuwa haitavumilia uchokozi wowote dhidi ya taifa lake.
Kutokana na shambulizi hilo, Iran imedokeza kuwa haina imani yoyote na Marekani katika ngazi zote, ikiwa ni pamoja na kijeshi na kidiplomasia, na kusisitiza kwamba, vitendo hivi vya Marekani vinakiuka waziwazi Mkataba wa Umoja wa Mataifa na makubaliano yanayohusiana ya kusitisha mapigano.
Hata hivyo, kwa upande wake, Marekani imeeleza kuwa mashambulizi hayo yalikuwa ya kujilinda dhidi ya vitisho katika eneo la bahari Hormuz.