Mgomo wa kitaifa wa matatu wasitishwa

Viongozi wa vyama vya wamiliki wa matatu wametangaza kusitisha mgomo huo kwa siku saba, wakitishia kuurejelea ikiwa hawataafikiana na serikali.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wamiliki wa magari ya uchukuzi wa umma maarufu kama matatu, wametangaza kusitisha mgomo wa kitaifa kwa wiki moja ili kutoa fursa kwa mazungumzo.

Viongozi wa vyama vya wamiliki wa matatu wametangaza kusitisha mgomo huo Jumanne kwa siku saba, ili kufanya mazungumzo na serikali.

Waziri wa Nishati Opiyo Wandayi amesema watafanya mazungumzo na wadau wa matatu ili kuafikia suluhu ya kudumu.

Serikali kupitia kwa EPRA ilitangaza kupunguza bei ya mafuta ya dizeli kwa shilingi 10 kwa lita moja, kufuatia mazungumzo ya Jumatatu jioni na wadau hao.

Hata hivyo, wadau wa matatu wameapa kurejelea mgomo endapo hawataafikiana na serikali baada ya wiki moja.

Mgomo huo ulioanza jana umelemaza shughuli za kawaida nchini kote, zikiwemo masomo na biashara.

 

Share This Article