Wakazi wa Nairobi kunufaika na huduma za uchukuzi zilizoimarika

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi, akutana na naibu waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza kuhusu bara Afrika, Lord Collins.

Wakazi wa Jiji la Nairobi watafaidika na huduma za uchukuzi wa reli baada ya Kenya na Uingereza kuazimia kutatua changamoto zinazokumba uchukuzi wa reli kwa utekelezaji mradi wa Nairobi Railways City.

Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi kupitia ukurasa wake wa X, alisema amekutana na naibu Waziri wa Mambo ya Nje Uingereza kuhusu bara Afrika, Lord Collins na balozi wa Uingereza humu nchini  Neil Wigan, ambapo walijadiliana kuhusu jinsi ya kufanikisha utekelezaji wa mradi huo.

Mudavadi alisema mradi huo utaimarisha usafiri katika jiji la Nairobi. Mradi huo utakuwa na kituo kikuu, njia mpya za mabasi ya kisasa ya uchukuzi wa abiria na vituo vya matatu, ambavyo vitarahisisha usafiri kwa wakazi kuingia na kutoka katikati mwa jiji la Nairobi.

Mudavadi alisema pia walijadili kuimarisha ushirikiano kati ya Kenya na Uingereza katika uwekezaji, teknolojia, usalama wa kikanda na kubuni nafasi za kazi, haswa kwa vijana hapa nchini .

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *