Klabu ya USM Alger ya Algeria(USMA), ilinyakua kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya pili, baada ya kuwashinda wenyeji Zamalek kutoka Misri ,penati 8-7, katika marudio ya fainali Jumamosi usiku jijini Cairo.
Zamaelek walishinda marudio hayo ya fainali bao moja kwa bila na ikabidi mechi iamuliwe kupitia penati baada ya USMA pia kushinda mkondo wa kwanza goli moja bila jawabu.
USMA walituzwa dola milioni 4 za Kimarekani kwa ushindi huo huku Zamelek, wakienda nyumbani na nusu ya kiwango hicho cha pesa.
USMA walikuwa wamenyakua kombe hilo kwa mara ya kwanza mwaka 2023 walipowalemea Yanga ya Tanzania fainalini.