Samba Boys na Simba wa Atlas watinga mwondoano Kombe la Dunia

Brazil waliongoza kundi C kwa alama 7 sawia na Morocco japo Samba Boys walio na ubora wa magoli.

Dismas Otuke
2 Min Read

Mabingwa mara tano wa Dunia Brazil almaarufu Samba Boys na Atlas Lions kutoka Morocco, zilifuzu kwa raundi ya 32 bora ya Kombe la Dunia baada ya kumaliza katika nafasi za kwanza na pili mtawalia.

Brazil waliongoza kundi C kwa alama sawa na Morocco, baada ya kuwalemea Scotland  mabao 3-0 nao Atlas Lions wakatoka nyuma mara mbili na kuwakomoa limbukeni Haiti magoli 4-2, katika mechi za mwisho mapema leo katika uga wa Atlanta,Marekani.

Vincious Junior alipachika magoli mawili katika kipindi cha kwanza naye Mateus Cunha, akaongoza jingine kipindi cha pili katika ushindi huo maridhawa ugani Miami.

Morocco upande wao waligutushwa na bao la dakika ya 10 la kujifunga kwa kipa Yassine Bonou na kuwapa Haiti, goli la kwanza na kusubiri hadi dakika ya 39, wakati nahodha Achraf Hakimi aliposawazisha.

Wilson Isidor aliwarejesha Haiti kifua mbele dakika 2, kabla ya mapumziko naye Ismael Saibari akasawazisha katika muda wa ziada kipindi cha kwanza.

Saibari aliweka historia kuwa mchezaji wa kwanza wa Afrika kufunga bao katika mechi tatu mtawalia za Kombe la dunia akiwa goli moja katika kila mechi na kufuta rekodi ya awali ya Mo Salah ya kufunga mabao 2 ,moja katika kila mchuano mtawalia.

Soufiane Rahmi na Gasime Yassine waliongeza goli moja kila mmoja kipindi cha pili na kuhitimisha ushindi huo wa Morocco wa 4-2.

Brazil waliongoza kundi C kwa alama 7 sawia na Morocco japo Samba Boys walio na ubora wa magoli.

Scotland ilimaliza ya ya tatu kwa alama 3.

Share This Article