Mchezaji nyota wa Algeria Riyad Mahrez ametangaza kustaafu rasmi kutoka soka ya kimataifa kufuatia kubanduliwa kwa timu yake kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Mahrez alikuwa nahodha wa timu yake katika mechi ya mwisho mapema Ijumaa walipoadhibiwa mabao 2-0 na Uswizi katika raundi ya 32.
Hadi kustaafu kwake, Mahrez aliye na umri wa miaka 35, ameichezea Desert Foxes mechi 119, kupachika magoli 40 na kuchangia mengine 45.
Wing’a huyo wa zamani wa Manchester City, anakumbukwa kwa kuiongoza Algeria kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2019 nchini Misri.
Algeria ilimaliza ya tatu katika kundi J la fainali za mwaka huu za Kombe la Dunia baada ya kupigwa na Argentina 3- 0, kuwashinda Jordan 2-1 na kutoka sare ya 3-3 na Austria.