Samia akutana na Rais wa Singapore, Tharman Shanmugaratnam

Rais Shanmugaratnam yuko nchini Tanzania kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili kwa mwaliko wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na Rais wa Singapore, Tharman Shanmugaratnam katika Ikulu ya Dar es Salaam.

Hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi wa serikali ya Tanzania na ile ya Singapore inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Rais Shanmugaratnam yuko nchini Tanzania kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili kwa mwaliko wa Rais Samia.

Katika ziara hiyo, mataifa hayo mawili yanatarajiwa kusaini makubaliano ya ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo ya kidiplomasia ambapo Singapore itafungua ubalozi wake nchini Tanzania

Share This Article