Rais Xi wa China kufanya mazungumzo na Trump

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa viongozi hao kukutana mwaka huu baada ya Rais Trump kufanya ziara nchini China mwezi Mei mwaka huu.

Martin Mwanje
1 Min Read
Marais Donald Trump wa Marekani na Xi Jinping wa China / Picha kwa hisani ya Xinhua

Rais wa China Xi Jinping atafanya ziara ya kitaifa nchini Marekani kuanzia kesho Jumatano hadi keshokutwa Alhamisi ili kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Donald Trump.

Hii ni kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China.

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa viongozi hao kukutana mwaka huu baada ya Rais Trump kufanya ziara nchini China mwezi Mei mwaka huu.

Akiwahutubia wanahabari, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Guo Jiakun aliwaambia wanahabari kuwa, miongoni mwa mambo mengine, viongozi hao wawili watabadilishana maoni kuhusu masuala muhimu ya kimataifa.

Aliahidi kuwa China itafanya kazi na Marekani ili kuboresha uhusiano unaonufaisha pande hizo mbili na unaozingatia uthabiti wa kimkakati.

Teknolojia ya akili unde, AI ni miongoni mwa masuala yanayotarajiwa kutawala mazungumzo kati ya Marais Xi na Trump kwenye mazungumzo yao wakati nchi zao zikionekana kuimarisha ushindani katika nyanja hiyo.

Share This Article