Chama cha Wanasheria Nchini Kenya, LSK, kimetangaza kuwa ujio wa wiki ya ufahamu wa sheria ya mwaka 2026.
Kulingana na bango kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii, LSK ilielezea kwamba mchakato huo utaandaliwa tarehe 26 hadi 30 Oktoba 2026, chini ya kaulimbiu, “Mawakili wa Jamii: Kuziba Pengo Kati ya Wananchi na Haki”.
Mpango huu wa kila mwaka, wa muda wa wiki moja, utafanyika katika matawi yote manane ya LSK pamoja na vituo vya Mahakama Kuu kote nchini.
Lengo lake ni kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu sheria na kuwasaidia kuelewa haki na wajibu wao chini ya sheria za Kenya.
Wakati wa tukio hilo, mawakili watatoa ushauri wa kisheria bila malipo kwa umma.
Wataendesha pia kliniki maalum za msaada wa kisheria na kutoa elimu ya uraia kuhusu masuala muhimu kama vile sheria ya madai, sheria ya jinai na sheria ya familia.
Aidha, kutakuwepo na makundi yatakayozuru vituo vya kurekebisha tabia na magereza ili kutoa msaada muhimu wa kisheria kwa watu walioko kizuizini au wanaotumikia vifungo.