NTSA yawakamata watu 50 kwa kukiuka sheria za trafiki

Washukiwa hao wanatarajiwa kufungulia mashtaka katika Mahakama za Milimani.

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu 50 wakamatwa kwa kukiuka sheria za trafiki Nairobi.

Mamlaka ya Uchukuzi na Usalama Barabarani (NTSA), imewakamata watu zaidi ya 50 kwa kukosa kutumia madaraja ya watembeaji kwa miguu kuvuka barabara.

Watu hao walikamatwa Jumatano wakati wa operesheni iliyotekelezwa na mamlaka hiyo katika eneo la Allsops kwenye barabara kuu ya Thika dhidi ya wanaokosa kutumia madaraja ya wanaotembea kwa miguu.

Washukiwa hao wanatarajiwa kufunguliwa mashtaka katika mahakama za Milimani.

Operesheni hiyo ni sehemu ya kampeni ambayo imekuwa ikiendelea katika muda wa wiki tatu zilizopita kukabiliana na uvukaji hatari wa barabara ambao husababisha ajali.

Siku ya Jumatatu, watembea kwa miguu 53 waliokosa kutumia daraja la Transami, katika mtaa wa Pipeline.

Mnamo siku ya Jumanne, maafisa wa NTSA walitekeleza operesheni sawia na hiyo katika daraja la wanaotembea kwa miguu la Mutindwa, ambapo watu kadhaa walikamatwa.

Mamlaka hiyo imetoa wito kwa wananchi kutumia madaraja ya wanaotembea kwa miguu kuvuka barabara kila wakati, ikisisitiza kuwa uzingatiaji wa sheria za trafiki ni muhimu katika kuimarisha usalama barabarani.

TAGGED:
Share This Article