Watu 131 wafariki kutokana na Ebola DRC

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu 131 wafariki kutokana na mlipuko mpya wa Ebola nchini DRC.

Takriban watu 131 wamethibitishwa kufariki kutokana na mlipuko mpya wa ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Kulingana na maafisa, maambukizi 513 yameripotiwa nchini humo.

Maafisa hao pia wamethibitisha kuwa maambukizi ya ugonjwa huo sasa yameenea hadi katika maeneo mengine ya taifa hilo yakiwa ni pamoja na Butembo Kaskazini mwa Kivu, na Goma.

Kituo cha Afrika cha kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Afrika CDC) kimesema kifo kimoja na visa viwili vimethibitishwa nchini Uganda.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza mlipuko huo wa Ebola kuwa dharura ya kimataifa.

Serikali ya DRC imewahakikishia raia kwamba makundi yake ya dharura yanajizatiti kufuatilia na kuchunguza walioambukizwa ugonjwa huo, huku ikiwataka wawe watulivu.

TAGGED:
Share This Article