Hamas yawaachilia huru mateka watatu wa Kiyahudi

Tom Mathinji and BBC
1 Min Read
Hamas imewaachilia huru mateka watatu wa kiyahudi.

Kundi la Hamas limewaachilia huru mateka watatu wa Kiyahudi kutoka Israeli huko Gaza, kwa kubadilishana na wafungwa wa Kipalestina waliokamatwa Israeli.

Eli Sharabi, Ohad ben Ami na Or Levy wamekabidhiwa kwa jeshi la Israeli.

Wanafamilia wa mateka hao wamesema kwamba wanaume hawa wanaonekana kuwa katika hali mbaya kiafya.

Waisraeli walikusanyika kwenye uwanja uliofahamika kama Hostages Square huko Tel Aviv ili kushuhudia kuachiliwa kwa wanaume hao.

Zaidi ya wafungwa 180 wa Kipalestina wanaachiliwa katika magereza ya Israeli chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas ambayo yalianza tarehe 19 Januari.

Katika hatua ya kwanza ya makubaliano, mateka 33 wa Kiyahudi wanatarajiwa kuachiliwa huru.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *