Kenya yanakili kisa kipya cha ugonjwa wa Mpox

Tom Mathinji
1 Min Read
Kenya yanakili kisa kipya cha Mpox.

Wizara ya Afya imethibitisha kisa kipya cha ugonjwa wa Mpox katika kaunti ya Makueni, na kufikisha idadi jumla ya visa vya ugonjwa huo hapa nchini 38.

Kupitia kwa taarifa Jumamosi, Katibu katika wizara ya afya Mary Muthoni, alisema ugonjwa huo sasa umeenea katika kaunti 12, huku Nakuru ikiongoza kwa  kunakili visa 10, ikifuatwa na Mombasa ikiwa na visa 8 nayo  Busia ikiwa ya tatu kwa kunakili visa vinne.

Nairobi, Kajiado, Bungoma, Taita Taveta, Kericho, Makueni, na  Kilifi, zimenakili visa viwili kila kaunti, nazo Kiambu na Uasin Gishu zikiwa na kisa kimoja kila kaunti.

Kulingana na Muthoni, watu 255 waliotangamana na watu 38 waliothibitishwa kuwa na ugonjwa huo, wametambuliwa ambapo 246 kati yao wametengwa kwa uangalizi kwa muda wa siku 21 huku hao wengine wakiendelea kuchunguzwa.

Hadi kufikia sasa, jumla ya watu Milioni 3.2 wamechunguzwa katika viwanja vya ndege na maeneo mengine ya mpakani, huku serikali ikiendelea na juhudu za kudhibiti ugonjwa huo.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *