Maafisa wawili wa Polisi wakamatwa kwa madai ya kushiriki ufisadi

Wawili hao ni Maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai katika afisi za kaunti ndogo ya Kipkelion, kaunti ya Kericho.

Tom Mathinji
1 Min Read
Maafisa wawili wa polisi wakamatwa kwa madai ya kushiriki ufisadi.

Tume ya Maadili na kukabiliana na Ufisadi (EACC), imewakamata Maafisa wawili wa Polisi kwa madai ya kuitisha na kupokea hongo.

Kulingana na taarifa ya tume hiyo, wawili hao ni Maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai katika afisi za kaunti ndogo ya Kipkelion, kaunti ya Kericho.

Washukiwa hao Corporal Wesley Korir na Corporal Christopher Maina, wanadaiwa kuitisha shilingi 500,000 kutoka kwa mlalamishi ili wafutilie mbali kesi ya mauaji dhidi yake.

Baada ya uchunguzi wa awali, wawili hao walikamatwa baada ya tume hiyo kutekeleza operesheni na kuwafumania wakipokea shilingi 120,000.

Baada ya kuandikisha taarifa,  waliachiliwa kwa dhamana ya shilingi 30,000 kila mmoja wakisubiri kukamilishwa kwa uchunguzi wa kisa hicho.

Kupitia ukurasa wa X, EACC ilirejelea kujitolea kwake kukabiliana na ufisadi katika sekta zote, ikitoa wito kwa wananchi kuripoti visa vyovyote vya ufisadi.

TAGGED:
Share This Article