Watatu wafariki kwenye ajali Machakos

radiotaifa
1 Min Read
Picha ya awali

Watu watatu walipoteza maisha yao mapema leo Jumatatu katika eneo la Ekati kuelekea sokoni Mutituni, kaunti ya Machakos.

Akithibitisha ajali hiyo,  Naibu wa Chifu wa lokesheni ya Kasinga Fredrick Kitonga ameeleza kuwa ilitokea baada ya pikipiki iliyokuwa imewabeba watu 5 kugongana na gari dogo la abiria saba aina ya Maroute.

Abiria watatu waliokuwa kwenye pikipiki hiyo walipoteza maisha yao papo hapo.

Boda boda hiyo ilikuwa imetoka eneo la sokoni Mutituni kuelekea mjini Machakos ilipogongana na gari hilo lililokuwa likitokea mjini Machakos.

Wengine wawili waliohusika kwenye ajali hiyo walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Machakos level 5.

Taarifa ya Jonathan Musau 

Share This Article