Mkurugenzi wa Mashitaka ya Umma Renson Igonga, amekariri kujitolea kwa afisi yake kudumisha uzingatiaji wa seria na kulinda nidhamu ya umma.
Igonga alisisitiza kuwa hatasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wale wanaotoa semi za chuki, uchochezi au uhuni ambao unatishia usala, amani na mshikamo wa kijamii.
“Uzingatiaji sheria lazima udumishwe kila wakati. Kama mkurugenzi wa mashtaka nitakabiliana vilivyo na watu ambao wanachochea jamii, wanaohujumu utulivu wa umaa na kuhatarisha usalama wa wananchi,” alisema Igonga.
Alisisita kuwa uhuru wa kujieleza ni sharti utekelezwe kwa uwajibikaji na kuzingatia sheria.
Igonga aliyasema hayo alipoungana na Jaji Mkuu Martha Koome kwenye ziara katika kaunti ya Kakamenga kujadiliana na maafisa wa serikali ya kaunti hiyo, wanachama wa watumiaji wa mahama na maafisa wa mahakama kuhusu maswala yanayoathiri utekelezaji haki.
Ziara hiyo ilitoa fursa kwa wadau kujadili changamoto zinazokabili sekta ya utoaji haki, na kuimarisha ushirikiano na wadau wa mashinani kuimarisha huduma za utoaji haki katika kaunti hiyo.