Ni afueni kwa Mbunge wa Emuhaya Omboko Milemba baada ya mahakama ya wafanyakazi kusimamisha kutimuliwa kwake katika wadhfa wa mwenyekiti wa Chama cha walimu wa shule za sekondari na vyuo nchini Kenya-KUPPET.
Akitoa uamuzi huo siku ya Alhamisi Jaji Monicah Mbaru alisema amesitisha uamuzi wa kesi hiyo iliyowasilihswa na Christine Osio kusubiri uamuzi wa kesi sawia iliyowasilishwa awali .
Jaji Mbaru alisema endapo atatoa uamui kabla ya kesi za awali kuamuliwa huenda ukaathiri uamuzi wa kesi hizo na pia kesi sijazo.
Asio alienda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi wa KUPPET ulioandaliwa Aprili 18 mwaka huu ambapo Milemba alihifadhi kiti chake.
Aidha,kesi hiyo inahoji uhalali wa Milemba kushikilia afisi hiyo na pia kiti cha Ubunge.
Kesi hiyo pia inataka matokeo ya uchaguzi huo kutupiliwa mbali na uchaguzi mpya kuandaliwa.