Shirika la ndege la Tanzania litaanzisha safari za moja kwa moja zinazounganisha Dar es Salaam, Zanzibar hadi Mosocw, Urusi kuanzia Julai 2 mwaka huu.
Akitangaza hayo Ijumaa iliyopita akiwa nchini Urusi, Rais Samia Suluhu Hassan alisema hatua hiyo inalenga kuimarisha utalii, biashara na ushirikiano baina ya Tanzania na Urusi.
Urusi ilisema usafiri huo utapiga jeki shughuli za kibiashara ikizingatiwa kuwa Tanzania ni mshirika mkubwa wa kimkakati.
Haya yaliafikiwa wakati wa ziara ya siku tatu ya Rais Samia nchini Urusi ambapo walifanya mazungumzo na Rais Vladimir Putin.