Kipchoge aunga mkono kampeni ya kuwafaa watoto walemavu

Kipchoge alitangaza kujiunga na kampeni hiyo siku ya Alhamisi alipomtembelea Panther  afisini mwake.

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa wa Olimpiki katika marathon Eliud Kipchoge ameunga mkono kampeni ya kuchangisha shilingi milioni 100 kuwanunulia viti vya magurudumu watoto wanaoishi na ulemavu.

Kampeni hiyo inayoongozwa na mwanzilishi wa shirika la Hope Mobility Kenya Michael Panther,itachangisha pesa hizo kupitia kwa kushiriki makala ya mwaka huu ya mbio za Standard Chartered Nairobi Marathon zilizoratibiwa kuandaliwa Oktoba 25.

Panther anayeishi na ulemavu atashiriki mbio za kilomita 42 akiwa mshiriki wa kwanza mwenye ulemavu kushiriki marathon humu nchini.

Kipchoge alitangaza kujiunga na kampeni hiyo siku ya Alhamisi alipomtembelea Panther  afisini mwake.

Kulingana na maelewano hayo, pesa zitakazokusanywa zitawezesha Hope Mobility Kenya, kutengeza viti vya magurudumu kwa watoto walemavu.

Share This Article