Kindiki awasili Tanzania kwa mkutano wa Afrika kuhusu miundombinu

Tom Mathinji
1 Min Read
Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki awasili Tanzania kwa mkutano wa kanda kuhusu miundombinu.

Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki, amewasili nchini Tanzania kuhudhuria mkutano wa Afrika kuhusu miundombinu na mkutano wa washikadau wa AFRICA50 utakaoandaliwa Dar es Salaam.

Kindiki atamwakilisha Rais William Ruto kwenye mikutano hiyo miwili ya ngazi za juu, itakayowaleta pamoja viongozi wa Afrika, wabuni sera, wawekezaji na washirika wa kimaendeleo kujadili ufadhili wa miundombinu na uwekezaji barani Afrika.

Mkutano kuhusu miundombinu unalenga kuangazia mbinu za kuchochea maendeleo ya miundombinu kupitia ushirikiano wa serikali na sekta za kibinafsi, ufadhili wa uvumbuzi na kuimarisha ushiriki wa sekta za kibinafsi.

Kwa upande mwingine mkutano wa washikadau wa  AFRICA50, utapigia kurunzi hatua zilizopigwa na kutoa mwongozo wa kimkakati.

Share This Article