Wakenya milioni 1.3 wamejisajili Boma Yangu, 18,000 wametengewa nyumba

Martin Mwanje
1 Min Read

Jumla ya Wakenya milioni 1.37 wamejisajili kwenye mfumo wa Boma Yangu wakati wakilenga kuwa wamiliki wapya wa nyumba nchini. 

Wakenya zaidi 18,000 tayari wametengewa nyumba chini ya mfumo baada ya kutimiza vigezo vilivyowekwa ikiwa ni pamoja na kutoa malipo ya awali.

Mfumo wa Boma Yangu ndio unaotumiwa kujisajili na wanaopania kuwa wamiliki wa nyumba ili kutengewa nyumba za ghamara ya bei nafuu.

Rais William Ruto anasema kwa sasa, nyumba 313,000 zinaendelea kujengwa katika kaunti zote 47 nchini huku zingine zikiwa tayari zimemalizwa kujengwa.

“Nyumba hizi hazihusu tu familia zinazopokezwa funguo, zinahusu pia mamilioni ya Wakenya wanaopata kipato wakizijenga, viwanda vinavyotengeneza saruji na nyenzo zingine za ujenzi,” alisema Ruto.

Alisema mpango huo wa nyumba za gharama nafuu umebuni nafasi za ajira milioni 1.1 huku wahandisi, wasanifu majengo, mafundi bomba na waashi miongoni mwa wengine wakifaidika.

 

 

 

Share This Article