Serikali ya Kenya imefanikiwa kupiga dafrau jinamizi la uhaba wa walimu uliokuwepo kabla ya kuingia madarakani mwaka 2022.
Rais William Ruto amesema kulikuwa na uhaba wa walimu 116,000 kabla ya serikali yake kuchukua hatamu za uongozi, uhaba ambao sasa umeshughulikiwa.
“Katika kipindi cha miaka minne, tumeajiri walimu 100,000 na ninajiandaa kuajiri walimu wengine 20,000 mwezi ujao,” alisema kiongozi wa nchi.
“Wazazi katika shule nyingi walikuwa wakitoa pesa za kuwalipa walimu walioajiriwa na Bodi za Usimamizi wakati wakigharimia mahitaji ya ziada ya madarasa na vituo vya mafunzo.”
Hali hiyo sasa imebadilika wakati Rais Ruto akisema uwekezaji unaofanywa na utawala wake unaboresha ubora wa elimu wakati kwa taratibu ukipinguza hitaji la Wakenya kufadhili elimu.
Aliyasema hayo wakati akihutubia taifa kutoka majengo ya bunge.
Ruto akiongeza kuwa katika kipindi cha miaka minne ambayo serikali yake imekuwa madarakani, wamejenga madarasa 23,000 na wanajenga na kuweka vifaa kwenye maabara 1,600.
Kulingana naye, vituo hivi vitasaidia kwa kiwango kikubwa katika kupanua upatikanaji wa elimu na kuipunguzia jamii shinikizo la kufadhili vituo muhimu vya mafunzo.