EPRA yaongeza bei ya bidhaa za mafuta

Tom Mathinji
1 Min Read

Halmashauri ya Kudhibiti Nishati na Petroli (EPRA), imetangaza nyongeza ya bei ya bidhaa za mafuta itakayotekelezwa kuanzia Mei 15, hadi Juni 14, 2026.

Kulingana na bei hizo mpya, Lita moja ya Super Petrol imeongezeka kwa shilingi 16.65,bei ya Diesel ikapanda kwa shilingi 46.29 kwa Lita, huku bei ya mafuta taa ikikosa kubadilika

Jijini Nairobi, Lita moja ya mafuta ya mafuta ya Super Petrol itauzwa shilingi 214.25, Diesel shilingi 242.92 huku Lita moja ya mafuta taa ikiuzwa  152.78.

Kulingana na EPRA, bei hiyo mpya inajumuisha ushuru husika.

Hata hivyo, serikali imetangaza ruzuku kupitia hazina ya maendeleo ya Petroli, ikilenga kutumia shilingi bilioni 5 ili kuwakinga wakenya dhidi ya bei za juu za Diesel na Mafuta Taa.

Bei hizo mpya zitaanza kutekelezwa Mei 15 na utadumu Kwa siku 30.

TAGGED:
Share This Article