Chuo Kikuu cha Moi kuwapiga kalamu Wahadhiri 75

UASU inasema chuo hicho kinatumia hali ya uhaba wa pesa unaokikabili  kuwafurusha Wahadhiri wenye tajriba.

Dismas Otuke
1 Min Read

Chuo Kikuu cha Moi kimetangaza kuwa kitawatimua Wahadhiri waandamizi 75 huku kikitangaza kujaza nafasi zao na Wahadhiri wasio wa kudumu.

Hatua hiyo imekilazimu Chama cha Wahadhiri wa Vyuo Vikuu vya Umma nchini (UASU) kukimbilia mahakamani kupinga hatua hiyo.

UASU inasema chuo hicho kinatumia hali ya uhaba wa pesa unaokikabili  kuwafurusha Wahadhiri wenye tajriba.

Chuo Kikuu cha Moi kimeanza mchakato wa kuwatimua Wahadhiri wa kudumu na wenye tajriba huku kikiwaajiri Wahadhiri wasio wa kudumu.

Share This Article