Sawe ajiondoa kutetea taji ya Berlin Marathon kutokana na jeraha

""Ni kwa masikito makubwa imebidi niwajuze kuwa nimelazimika kujiondoa kwa mbio za mwaka huu za Berlin Marathon kutokana na jeraha,"akasema Sawe

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa mtetezi na mshikili wa rekodi ya Dunia ya Marathon Mkenya Sabastian Sawe, amejiondoa kutetea taji ya mbio za Berlin mwaka huu kutokana na jeraha.

Sawe aliyeweka rekodi mpya ya dunia ya saa 1 dakika 59 na sekunde 30 aliposhinda mbio za London Marathon mwezi Aprili mwaka huu alikuwa analenga kutetea taji ya Berlin Marathon aliyotwaa mwaka uliopita.

“”Ni kwa masikito makubwa imebidi niwajuze kuwa nimelazimika kujiondoa kwa mbio za mwaka huu za Berlin Marathon kutokana na jeraha,”akasema Sawe

“Nilikuwa natazamia kupata matokeo mazuri katika mbio za Berlin wakati ningezikamilisha ,ilikuwa njia pekee ya kurudisha shukran kwa waandalizi wa mbio hizi ambao wameshikilia mkono sana.” akongeza Sawe

Kujiondoa kwa Sawe kuna waacha bingwa wa Dunia Gabriel Geay kutoka Tanzania,Guye Adola na Gateneh Molah wa Ethiopia pamoja na Wakenya Rochard Yator na Erick Sang miongoni mwa washiriki wengine.

Share This Article