Idadi ya walioangamia Nepal kwa mafuriko yapita 270

Kulingana na bodi ya Utalii nchini Nepal,Watalii  644 hawajulikani waliko wakiwemo raia wa kigeni  517  na raia  127 wa Nepal .

Dismas Otuke
1 Min Read

Mili 270 imepatikana katika eneo lililokumbwa na mafuriko nchini Nepal huku raia wengine 288 wa India, wakiwa hawajulikani waliko kufuatia mkasa huo katika eneo la Tibet.

Rais wengine 21 wa India waliokuwa kwenye safari ya kihujaji waliokolea .

Makundi ya uokoaji yaliendeleza shughuli ya kutafuta manusura na mili katika mpaka wa Nepal na Uchina, kufuatia mafuriko hayo yaliyowasomba watu na nyumba mapema Jumatano.

Zaidi ya watu 50 hawajulikani waliko katika eneo la Tibet wakiwemo raia wa kigeni .

Kulingana na bodi ya Utalii nchini Nepal,Watalii  644 hawajulikani waliko wakiwemo raia wa kigeni  517  na raia  127 wa Nepal .

 

 

Share This Article