Rais wa Marekani Donald Trump, amemteua mwanadiplomasia mkongwe Henry Wooster kuwa balozi wa Marekani nchini Kenya.
Kupitia kwa taarifa kutoka Ikulu ya White House Juni 1, 2026, Wooster alitajwa kuwa balozi wa Marekani nchini Kenya, huku uteuzi huo ukisubiri kuidhinishwa na bunge la Senate.
“Henry Wooster, kutoka Virginia, ambaye ni mwanachama wa huduma za nje ameteuliwa kuwa balozi wa Marekani katika Jamhuri ya Kenya,” ilisema taarifa hiyo.
Wooster, ni mwanadiplomasia mwenye uzoefu wa miaka mingi hususan katika sera za kimataifa na uhusiano wa mambo ya nje.
Awali ameshikilia nyadhifa kadhaa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani na jumbe za kidiplomasia kote duniani.
Vile vile aliwahi hudumu kama naibu mkuu wa ujumbe wa Marekani Jiji Paris Ufaransa na baadaye balozi wa Marekani nchini Jordan.