Ruto asaini mswada wa bajeti ya ziada 2024 kuwa sheria

Martin Mwanje
1 Min Read

Rais William Ruto ametia saini kuwa sheria mswada wa bajeti ya ziada 2024. 

Katika hafla iliyoandaliwa katika Ikulu ya Nairobi leo Jumatatu, Ruto pia ametia saini kuwa sheria mswada wa ugavi wa mapato 2024.

Anasema mswada wa bajeti ya ziada utaruhusu kutolewa kwa rasilimali zinazohitajika ili kuchochea ukuaji uchumi na kuboresha utendakazi wa serikali ya Kenya Kwanza.

Mswada huo unatenga rasilimali zaidi kwa ajili ya maendeleo na elimu ya sekondari na vyuo vikuu.

Kadhalika, unapunguza bajeti ya jumla kwa shilingi bilioni132, hatua ambayo Rais Ruto anasema inaashiria kujitolea kwa serikali kupunguza nakisi na madeni ya nchi.

Waliokuwepo wakati wa hafla ya utiaji saini wa miswada hiyo ni pamoja na Naibu Rais Rigathi Gachagua, Mwanasheria Mkuu Justin Muturi na Waziri wa Fedha Prof. Njuguna Ndung’u miongoni mwa wengine.

Website |  + posts
Share This Article