Mwanamume awaua wanawe wawili kabla ya kujitoa uhai Mai Mahiu

Tom Mathinji
1 Min Read
Mwanamume awaua wanawe wawili kabla ya kujitoa uhai Mai Mahiu.

Hali ya huzuni ilighubika eneo la Mai Mahiu, kaunti ndogo ya Naivasha baada ya mwanamume kuwaua wanawe wawili na kisha kujitoa uhai.

Inadaiwa kuwa mwanamume huyo aliwaua watoto hao kwa kuwawekea sumu kwenye uji nyumbani kwake Duka Moja kabla ya kujitia kitanzi baada ya kuzozana na mkewe.

Huzuni ilitanda nyumbani kwake huku marafiki na jamaa wakishangazwa na tukio hilo.

Mama wa watoto hao, Mary Karuku, alisema mumewe waliyetengana, alifika nyumbani kwao akiwa hayuko nyumbani na kuwapeleka watoto hao mahali ambako hakujulikani.

“Siku iliyofuatia niliamua kusafiri nyumbani baada ya simu yake kuzimika, nilifika na kupata amewaua watoto wanguwawili naye akajitoa uhai,” alisema Karuku.

Mwakilishi wadi wa zamani Eunice Mureithi, aliyetembelea familia hiyo, alitaja tukio hilo kuwa la kinyama na akatoa wito kwa watu walio na mizozo ya kifamilia kuizungumzia.

“Tunafahamu kuwa familia nyingi zinapitia changamoto, lakini ghasia na mauaji hayatatoa suluhu kwa changamoto hizo,” alisema Mureithi.

Polisi mjini Duka Moja walithibitisha tukio hilo wakisema miili hiyo mitatu imepelekwa katika chumba cha wafu  cha hospitali ya kaunti ya Narok.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article