Serikali ya Tanzania imetangaza kuondoa marufuku ya bidhaa za kilimo zinazoingizwa nchini humu kutokea mataifa ya Afrika Kusini na Malawi.
Tanzania ilitoa tangazo hilo Ijumaa iliyopita baada ya kusitisha uingizaji wa mazao ya kilimo kutoka nchini hizo kulipiza kisasi cha vikwazo ambavyo Afrika Kusini na Malawi ilikuwa imewekea mazao yake.
Nchini tatu ziliafikiana wiki jana kusuluhisha mzozo huo wa kibiahara ambao ulikuwa unahatarisha muungano wa SADC.
Malawi ilikuwa imesitisha uagizaji wa mbolea ya Tanzania, mpunga, tangawizi na unga wa mahindi huku Afrika Kusini ikipiga marufuku ndizi mbivu za kutoka.