Baraza la kitaifa la mitihani nchini (KNEC),limetangaza kutoa vyeti vya wanafunzi waliokalia mitihani ya kitaifa ya KCPE na KCSE mwaka 2023.
Kwenye taaria kwa umma ,KNEC imewashauri wanafunzi kufika shuleni ili kupokea vyeti vyao.
Aidha, wanyima imetoa onyo kwa walimu wakuu dhidi ya kuwanyima vyeti wanafunzi walio na malimbikizi ya karo.
Waziri wa Elimu Julius Ogamba mwezi uliopita alitoa amri kwa shule zote kuachilia vyeti vya wanafunzi walio na malimbikizi ya karo.