Timu ya taifa ya Kenya kwa wachezaji saba upande, Shujaa, imeondoka nchini leo kuelekea Los Angeles, Marekani, kwa mechi za mchujo kuwania kupashishwa ngazi kutoka mashindano ya msururu wa Dunia .
Mechi hiyo zitaandaliwa kati ya Mei 3 na 4, huku Kenya, wakifungua ratiba tarehe 3 dhidi ya Samoa, kabla ya kupambana na Ureno na Marekani Mei 4 kabla ya mechi za mwondoano.
Jumla ya timu 8 zilizogawanywa katika makundi mawili ya timu nne zinashiriki mchujo huo huku timu mbili bora kutoka kila kundi zikicheza nusu fainali.
Kenya ilijipata katika mashindano hayo ya mchujo baada ya kumaliza ya tisa katika mashindano ya mururu wa mwaka 2024/2025.