Kenya yaendeleza mazoezi Misri, kujiandaa kwa kipute cha AFCON

Kenya itafungua harakati za kuwania kombe hilo kundini B Mei mosi dhidi ya Morocco .

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya ya soka kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20, Rising Stars, imeendeleza mazoezi nchini Misri kujiandaa kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika zilizoanza jana.

Kenya itafungua harakati za kuwania kombe hilo kundini B Mei mosi dhidi ya Morocco .

Timu nyingine kundini B na Kenya ni Tunisia na Nigeria.

Kocha wa Kenya Salim Babu, ana imani kuwa vijana wake wamejiandaa vyema na wako tayari kwa mchuano wa ufunguzi licha ya kuwa wanashiriki kipute hicho kwa mara ya kwanza.

Timu nne bora kutoka kwa mashindano hayo zitafuzu kwa Kombe la Dunia nchini Colombia, mwishoni mwa mwaka huu, Tanzania .

Website |  + posts
Share This Article