Mshukiwa wa ulanguzi wa mihadarati afikishwa mahakamani

Tom Mathinji
1 Min Read
Mshukiwa wa ulanguzi wa mihadarati afikishwa mahakama ya JKIA.

Mwanamke anayeshukiwa kushiriki ulanguzi wa mihadarati amefikishwa katika mahakama ya Uwanja wa Ndege ya Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA).

Safia Burhan Marjan, alikamatwa baada ya maafisa wa usalama kufanya msako kwenye nyumba yake katika mtaa wa Raila mwishoni mwa wiki.

Kwenye msako huo, maafisa hao walipata gramu 462 za bangi na gramu 240 za dawa aina ya Cocaine.

Mahakama iliagiza mshukiwa huyo azuiliwe kwa siku nne, ili kuwapa maafisa wa usalama muda wa kukamilisha uchunguzi.

Hatua hiyo inajiri siku chache baada ya washukiwa sita wa Iran kukamatwa na mihadarati ya shilingi bilioni 8.2 katika pwani ya Mombasa.

Washukiwa hao walikamatwa siku ya Ijumaa katika bandari ya Kilindini kufuatia msako wa pamoja ya mashirika mbalimbali uliowezesha kukamatwa kwa vifurushi 769 vya dawa hiyo inayoshukiwa kuwa Methamphetamine yenye uzito wa kilo 1,024.

Website |  + posts
Share This Article