Jepchirchir, Jebet na Sawe kuwania tuzo ya mwaka ya Mwanariadha bora nje ya uwanja

Dismas Otuke
1 Min Read
TOKYO, JAPAN - SEPTEMBER 14: Peres Jepchirchir of Kenya poses with the flag after winning the gold medal during the Women's Marathon at day two of the World Athletics Championships Tokyo 2025 at National Stadium on September 14, 2025 in Tokyo, Japan. (Photo by Daniela Porcelli/Getty Images)

Bingwa wa Dunia katika marathon Peres Jepchirchir, mshikilizi wa rekodi ya Dunia ya Kilomita 10 Agnes Jebet Ngetich, na bingwa wa London na Berlin Marathon Sebastian Sawe ndio Wakenya waliochaguliwa kuwania tuzo ya Mwanariadha Bora wa mwaka katika mbio za nje ya uwanja.

Jepchirchir alishinda taji la tano la Dunia la marathon katika mashindano ya Riadha jijini Tokyo, Japani, Septemba mwaka huu.

Jebet naye aliweka rekodi ya dunia kwa wanawake pekee katika mbio za kilomita 10 na kuweka muda wa kasi wa tatu katika mbio za nusu marathoni aliposhinda Valencia half marathon siku ya Jumapili.

Wawili Hao wanawania tuzo hiyo pamoja na Tigst Assefa wa Ethiopia aliyemaliza wa pili katika mashindano ya Tokyo, bingwa wa kilomita 20 na 35 za matembezi Maria Perez wa Uhispania na bingwa wa Sydney Marathon Sifan Hassan kutoka Uholanzi.

Sawe alishinda London Marathon, na anawania tuzo hiyo pamoja na Caio Bonfim wa Brazil, Evan Dundee wa Canada, Yomif Kejelcha wa Ethiopia na Alphonse Felix Simbu wa Tanzania.

Website |  + posts
Share This Article