Lori la kubeba mafuta limelipuka na kuteketea katika eneo la Sachangwan, kwenye barabara ya Nakuru-Eldoret, usiku wa kuamkia leo Jumanne.
Shirika la Msalaba Mwekundu, limesema kwa sasa eneo hilo limefungwa kati ya Kibunja na Soilo, madereva wakitakiwa kutumia barabara mbadala hadi hali ya kawaida itakaporejea.
Kulingana na Shirika hilo, limewahudumia waathiriwa wawili wa mkasa huo, huku asasi mbalimbali za kushughulikia dharura, zikishirikiana na kufanikiwa kukabiliana na moto huo.
“Maafisa wetu waliwahudumia waathiriwa wawili wa mkasa huo,” lilisema Shirika la Msalaba Mwekundu kupitia ukurasa wa X.<
Kulingana na shirika hilo, maafisa hao wa kushughulikia dharura bado wanaendelea na shughuli za uokoaji.
Eneo la Sachangwan awali limenakili ajali kadhaa ambazo zimesababisha maafa na majeraha.