Uganda yathibitisha visa vipya sita vya Ebola

Maambukizi hayo yanafikisha jumla ya visa kuwa 15 na kifo kimoja, kulingana na Wizara ya Afya nchini humo.

Dismas Otuke
1 Min Read

Nchi jirani ya Uganda imethibitisha visa vipya sita vya maambukizi ya ugonjwa wa Ebola.

Maambukizi hayo yanafikisha jumla ya visa kuwa 15 na kifo kimoja, kulingana na Wizara ya Afya nchini humo.

Kama njia ya kudhibiti maamumbukizi, Uganda imefunga mipaka yake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na kusitisha usafiri wote wa raia wake kuelekea DRC.

Aidha, imezuia wageni kutoka DRC kuingia nchini humo.

Kwenye mkutano wao leo Jumatano, makatibu wa afya kutoka nchi za Afrika wametoa wito wa jitihada za pamoja ili kuzuia msambao wa ugonjwa wa Ebola barani humo.

 

 

Share This Article