Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi, almaarufu Bobi Wine, ametangaza kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao kwa mara ya pili.
Akitoa tangazo hilo siku ya Ijumaa, Wine aliye na umri wa miaka 43, amekashifu mataifa ya Ulaya kwa ukiukaji wa haki za kibinadamu.
Wine atashindana na Rais Yoweri Museveni, aliye na umri wa miaka 80, na anayetarajiwa kutangaza azma ya kutetea kiti chake.
Kiongozi huyo wa upinzani alimaliza wa pili kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2021, huku akikataa kukubali matokeo akidai wizi wa kura.