Kindiki: Serikali haitalegeza kamba kuangamiza pombe haramu

Prof. Kindiki alisema serikali itahusisha asasi mbali mbali kushughulikia utengenezaji na usambazaji wa vinywaji vyenye sumu.

Tom Mathinji
1 Min Read
Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki afanya ziara ya maendeleo kaunti ya Kiambu.

Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki amesema serikali haitalegeza kamba kwenye azma yake ya kusabaratisha utengenezaji na uuzaji wa pombe haramu nchini Kenya.

Akizungumza katika kaunti ya Kiambu siku ya Jumatatu, Kindiki alithibitisha kuwa serikali imeanzisha mchakato wa kuwagakua upya watengenezaji na wauzaji wa pombe, kuhakikisha pombe inayotengenezwa ni salama kwa matumizi ya binadamu.

Kulingana na Naibu huyo wa Rais, Leseni za watenegenezaji pombe zitachunguzwa  upya, ili kuhakikisha viwango vya afya na ubora wa hali ya juu vinazingatiwa.

Ili kufanikisha vita dhidi ya pombe haramu hapa nchini, Prof. Kindiki alisema serikali itahusisha asasi mbali mbali kushughulikia utengenezaji na usambazaji wa vinywaji vyenye sumu.

Aliyasema hayo alipokuwa akiwahutubia wananchi katika Soko la Nyambari, eneo bunge la Lari, Kaunti ya Kiambu, kwenye ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo kati kaunti ya Kiambu.

Kwnye ziara hiyo, Kindiki aliwahimiza wakenya kupinga ghasia za kisiasa na kulinda miradi ya maendeleo.

Share This Article