Jengo lililokuwa likijengwa katika barabara ya 9th Street mtaani Eastleigh, Nairobi, limeporomoka, huku watu kadhaa wakihofiwa kukwama kwenye vifusi vya jengo hilo. Hayo yametangazwa na Shirika la Msalaba Mwekundu.
Shirika hilo la Msalaba Mwekundu limesema limewapeleka maafisa wake kwa shughuli za uokoaji, huku Kamanda wa Polisi eneo la Nairobi Issa Mohamed, akidokeza kuwa maafisa zaidi wamewasili na wameanza za uokoaji.
Jengo hilo liliporomoka saa saba mchana, katika eneo lenye shughuli nyingi za uchukuzi.
Hata hivyo, maafisa wa usalama walilazimika kurusha vitoza machozi ili kuwatawanya wananchi waliofika katika eneo la mkasa na kutatiza shughuli za uokoaji zilizokuwa zikiendelea.
Idadi kamili ya waathiriwa, na chanzo cha kuporomoka kwa jengo hilo, bado havijabainishwa.