Uganda,Algeria zatua robo fainali Kombe la Afrika,Voliboli ya wanawake

Uganda imejikatia tiketi kwa awamu ya nane bora kufuatia ushindi wa seti 3-0 dhidi ya DR Congo za 25-16, 27-25 na 25-18

Dismas Otuke
1 Min Read

Uganda na Algeria zimejikatia tiketi kwa kwota fainali ya mashindano ya mpira  wa wavu barani Afrika kwa wanawake,mashindano yanayoendelea jijini Nairobi.

Uganda imejikatia tiketi kwa awamu ya nane bora kufuatia ushindi wa seti 3-0, dhidi ya DR Congo za 25-16, 27-25 na 25-18, katika mchuano wa raundi ya 16, uliopigwa Jumamosi katika ukumbi wa Kasarani.

Algeria pia walifuzu kwa robo fainali baada ya kuwalemea Senegal seti 3-0, katika mechi ya raundi ya 16 bora.

Algeria walisajili ushindi wa seti za 25-15, 25-17 na 25-16, na kujikatia tiketi kwa raundi ya nane bora.

Mechi zaidi za hatua ya 16 bora zitachezwa Jumapili .

Share This Article