Waziri wa nishati nchini Tanzania Deogratius Ndejembi, ameapishwa Jumamosi katika Ikulu ya Dodoma, kuwa Makamu Rais nchini Tanzania,akichukua nafasi ya Dkt.Emmanuel Nchimbi aliyeziulu.
Ndejembi amekula kiapo siku ya Jumamosi,siku moja tu baada ya bunge kuidhinisha uteuzi wake na Chama tawala cha Mapinduzi CCM,katika wadhfa huo.
Akihutubu punde baada ya hafla hiyo fupi,Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, alimtaka Ndejembi kutuamia umri wake mdogo na kutekeleza makujumu magumu ya afisi hiyo kwa hekima.
Ndejembi alipitishwa na wabunge wote 324, kuhudumu katuka nafasi hiyo huku mtangulizi wake aliyejiuzulu Dkt Nchimbi akitimuliwa katika chama cha CCM.