Kesi ya Lissu: Hoja za mwisho zasikilizwa

Mshtakiwa ambaye ni Mwenyekiti wa Kitaifa wa CHADEMA, alieleza mahakama kuwa matamshi aliyotoa hayatoshi kisheria kuthibitisha kosa la uhaini analoshtakiwa.

Marion Bosire
1 Min Read
Tundu Lissu, Kiongozi CHADEMA

Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam,inasikiliza mawasilisho ya mwisho ya hoja za upande wa utetezi na Jamhuri, katika kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu.

Mshtakiwa ambaye ni Mwenyekiti wa Kitaifa wa CHADEMA, alieleza mahakama kuwa matamshi aliyotoa hayatoshi kisheria kuthibitisha kosa la uhaini analoshtakiwa.

Lissu aliambia jopo la majaji watatu wanaosikiliza shauri hilo wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, kwamba alitoa kauli hizo ingawa amesisitiza kuwa kisheria kauli hizo hazitoshi kuthibitisha kosa la uhaini.

kiongozi huyo wa upinzani alisema hajawahi kuficha wala kukana kwamba alisema maneno hayo, akirejelea ukurasa wa 97 wa rekodi ya mahakama ya Kisutu tarehe 18-8-2025.

“Ni kweli nilisema maneno hayo kwenye vyombo vya habari wazi suala ni je hayo maneno yanatengeneza kosa la uhaini?” Aliuliza Lissu.

Tundu Lissu alisema maneno yanayotajwa kuwa uhaini ni yake na hakuyasema mara moja bali aliyasema mara kadhaa katika maeneo ya Mbeya, Songwe, Iringa, Songea, Njombe, Lindi na Mtwara.

Hatua hii ya uwasilishaji wa maelezo ya mwisho katika kesi hiyo imefikiwa ikiwa ni siku kadhaa baada ya kufungwa kwa hatua ya ushahidi wa pande zote mbili, upande wa utetezi na upande wa jamhuri.

Share This Article