Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen, amesema serikali inatekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo yote ya nchi, huku ikileta huduma za serikali karibu na wananchi.
“Tunatekeleza maendeleo katika pembe zote za nchi kupitia uwekezaji katika miundombinu kwa kupeleka huduma za serikali karibu na wananchi,” alisema Murkomen.
Murkomen alidokeza kuwa serikali inajizatiti kubuni fursa zitakazopiga jeki biashara ndogo na zile za kadri, kuwezesha jamii na kuimarisha maisha ya wananchi.
Aliyasema hayo Ijumaa kwenye hafla ya kuwezesha jamii katika eneo la Koitugum, kaunti ya Elgeyo-Marakwet.
Mpango huo utawanufaisha makundi ya wanawake na vijana kwa kuwapa fedha za kuanzisha biashara, kubuni nafasi za ajira na kuimarisha maisha.
“Kupiga jeki makundi haya ya vijana na wanawake, kunawapa fursa mwafaka ya kupanua biashara zao,” alisema Murkomen.