Helikopta yaanguka Kericho, majeruhi wakimbizwa hospitalini

Martin Mwanje
1 Min Read

Helikopta moja imeaanguka katika uwanja wa Kericho Golf Club, kaunti ya Kericho. 

Helikopta hiyo, nambari ya usajili 5Y-FSK, ilianguka leo Jumatatu mchana baada ya kujaribu kupaa mara kadhaa.

Uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha kuanguka kwa helikopta hiyo.

Inasemekana ndege hiyo ilikuwa na watu sita wakati wa ajali hiyo.

Majeruhi, akiwemo rubani wa helikopta hiyo, wamekimbikizwa hospitalini kwa matibabu.

Katibu katika Wizara ya Mazingira Festus Ng’eno ni miongoni mwa watu wanaosemekana walikuwa wameabiri ndege hiyo.

 

 

Share This Article