Kamanda wa Polisi katika kaunti ya Mombasa Stella Jerono amethibitisha kisa cha ufyatuaji risasi kilichohusisha mlinzi wa Gavana wa Mombasa Abdullswamad Sherrif Nassir na vijana.
Kisa hicho kilitokea leo Ijumaa wakati wa mkutano uliofanyika katika uwanja wa Bomu, kaunti ndogo ya Changamwe.
Vijana hao walidaiwa kupigwa risasi mkutano huo ulipogeuka kuwa wenye vurugu walipoanza kutoa kaulimbiu za “one-term”. s
Jerono amesema vijana watatu walipata majeraha ya risasi na kukimbizwa katika hospitali ya Mikindani kabla ya kuhamishiwa ile ya Mafunzo na Rufaa ya Pwani ili kutibiwa.
Ameashiria kuwa uchunguzi kuhusiana na kisa hicho umeanzishwa ili kuwawajibisha wahusika.
Taarifa ya Sadiq Hassan