Serikali yatenga bilioni 1.4 kwa usambazaji umeme Busia

KBC Digital News
1 Min Read

Waziri wa Nishati Opiyo Wandayi anasema serikali imetenga shilingi bilioni 1.46 za kuunganisha umeme katika zaidi ya nyumba 17,000 katika kaunti ya Busia. 

Akizungumza katika vijiji vya Mabunge na Muramia katika kaunti ndogo ya Nambale, Wandayi amesema hatua hiyo inalenga kupanua upatikanaji wa umeme na kuboresha mapato ya wakazi wa eneo hilo.

Aliongeza kuwa eneo bunge la Nambale limepokea shilingi milioni 350 za kuwezesha uunganishaji wa umeme kwa nyumba zipatazo 280, akiuelezea mradi huo kama utakaoleta manufaa kwa wakazi.

Kulingana na Wandayi, upatikanaji wa umeme utaunga mkono biashara, na kuboresha masomo na ubora wa maisha kwa jumla katika jamii husika.

Ni kauli zilizoungwa mkono na mbunge wa Nambale Geoffrey Mulanya na Mwakilishi wa Wanawake wa kaunti hiyo Catherine Omanyo.

Wote hao wakifurahia uwekezaji wa serikali katika kuwaunganishia wakazi umeme, uwekezaji waliosema utabuni fursa za uwezeshaji wa kiuchumi wakati ukiunga mkoni maendeleo mashinani.

Taarifa ya Sayyid Abdalla 

Share This Article